RIADHA-KENYA

Polisi nchini Kenya wamkamata afisa wa michezo kwa kuficha sare za wachezaji

Makamu mwenyekiti wa kamti ya Olimpiki ya Kenya, Pius Ochieng na Francis Paul wakiwa mahakamni jijini Nairobi, 29 Agosti, 2016.
Makamu mwenyekiti wa kamti ya Olimpiki ya Kenya, Pius Ochieng na Francis Paul wakiwa mahakamni jijini Nairobi, 29 Agosti, 2016. REUTERS/Thomas Mukoya

Maafisa wa usalama nchini Kenya wanamshikilia Ben Ekumbo, naibu kiongozi wa ujumbe wa kikosi cha wachezaji wa Kenya kilichokwenda kushiriki katika Michezo ya Olimpiki mwaka huu nchini Brazil.

Matangazo ya kibiashara

Hatua hii imekuja baada ya polisi kuvamia nyumbani kwake siku ya Jumatatu na kupata sare za wanamichezo zilizokuwa zimefichwa baada ya kupewa ufadhili na kampuni ya Marekani ya Nike.

Ripoti zinasema kuwa polisi, waliamua kuvunja mlango nyumbani kwa Ekumbo na kuzipata jezi hizo, baada ya kukataa kuufungua mlango.

Ekumbo pia ni Mwenyekiti wa Shirikisho la kuogelea nchini Kenya na amefikishwa Mahakamani jijini Nairobi kufunguliwa mashtaka.

Viongozi wengine wa Kamati ya Kitaifa ya Michezo ya Olimpiki nchini humo wakiongozwa na aliyekuwa Mkuu wa ujumbe ;

Stephen Soi, Meneja Pius Ochieng, Katibu Mkuu Jenerali Francis Paul, na Mwekahazina Fridah Shiroya tayari wamefunguliwa mashtaka ya matumizi mabaya ya Ofisi na usimamizi mbaya wa kikosi cha Kenya.

Mbali na hili, maafisa katika Wizara Michezo wanatuhumiwa pia kufuja Mamilioni ya fedha za Kenya zilizokuwa zimetengwwa kuwaanda wachezaji hao.