ENGLAND-GERRARD

Kiungo wa zamani wa Liverpool na timu ya taifa ya England, Steven Gerrard atangaza kustaafu soka

Mchezaji wa LA Galaxy, Steven Gerrard ambaye ametangaza kustaafu soka
Mchezaji wa LA Galaxy, Steven Gerrard ambaye ametangaza kustaafu soka Isaiah J. Downing-USA TODAY Sports

Nahodha wa zamani wa klabu ya Liverpool na timu ya taifa ya England, Steven Gerrard, ametangaza kustaafu soka na kumaliza miaka 19 ya maisha yake ya kucheza soka. 

Matangazo ya kibiashara

Gerrard mwenye umri wa miaka 36, ameichezea klabu ya Liverpool mara 710, akishinda mataji manne, lakini alijiunga na klabu ya Marekani ya MLS LA Galaxy mwaka 2015.

Gerrard anakuwa mchezaji wa nne katika historia ya wachezaji waliowahi kuichezea timu ya taifa ya England mara nyingi zaidi, ambapo ameitumikia mara 114 na kuiongoza timu yake mara tatu katika michuano 6 mikubwa.

Kiungo huyu ameitumikia klabu ya Liverpool kama nahodha kwa miaka 12 ambapo alipata umaarufu mkubwa wakati alipoiongoza timu yake kutwaa taji la klabu bingwa barani Ulaya, UEFA mwaka 2005, baada ya kutoka nyuma na kuifunga klabu ya AC Milan katika fainali ya aina yake.

Licha ya kuwa ameshawahi kushinda mataji mawili ya kombe la FA, mataji matatu ya kombe la ligi na UEFA, anamaliza maisha yake ya soka bila ya kuwa amewahi kutia mkono wake katika kombe la ligi kuu ya England "Premier League".

Aliondoka kwenye klabu hiyo mwaka 2015 baada ya miezi 12 ya kujaribu kutafakari maisha yake ya soka na vijogoo vya jiji Liverpool, ambapo kubwa ni mwaka mbaya aliokuwa nao kwenye klabu yake.

Gerrard alimanusura ashinde kwa mara ya kwanza taji la ligi kuu ya England mwaka 2014, lakini kufungwa kwa timu yake na klabu ya Chelsea kwenye dimba lake la nyumbani, kukaikosesha timu yake ubingwa na Manchester City msimu huo kutwaa taji.