BRAZIL-SOKA

Wachezaji wa timu ya soka ya Brazil waangamia baada ya ndege yao kuanguka

Ndege iliyokuwa imebeba timu ya soka ya Brazil ya Chapecoense ilianguka Jumatatu usiku karibu na mji wa Colombia wa Medellin. Ndege hii ilikuwa amebeba jumla ya abiria 72 na wafanyakazi 9 wa ndege hiyo. Idadi rasmi ni ya vifo vya watu 76 na watano wamenusurika.

Jamaa ndugu na marafiki wakiomboleza baada kusikia habari ya ajali ya ndege iliyokuwa na wachezaji wa Chapecoense.
Jamaa ndugu na marafiki wakiomboleza baada kusikia habari ya ajali ya ndege iliyokuwa na wachezaji wa Chapecoense. REUTERS/Fredy Builes
Matangazo ya kibiashara

"Habari hii imethibitishwa, Ndege yenye namba za usajili CP2933 iliyokua ikibeba timu ya soka ya ChapecoenseReal. Inaonekana kuwa kuna watu ambao wamenusurika, " afisa wa uwanja wa ndege wa Jose Maria Cordova ameandika kwenye Twitter.

Kwa mujibu wa chanzo kimoja, ndege hiyo iliyokua ikitokea Bolivia na abiria 72 pamoja na wafanyakazi 9 ilianguka katika eneo la Cerro Gordo, katika wilaya ya La Union. Watu sita pekee ndio wamenusurika.

"Usafiri wa nja ya barabarani ndio pekee ambao unatumiwa kwa kufika kwenye eneo la tukio, kilomita 50 kutoka mji wa Medellin, kwa sababu ya "hali ya hewa," mamlaka ya uwanja wa ndege imesema katika taarifa yake.

"Inavyoonekana, ndege ilianguka ya kukausha mafuta," Elkin Ospina, Meya wa wilaya ya La Ceja, mji uliokaribu na wilaya ya La Union ameliambia shirika la habri la AFP. Amesema maafisa wa huduma za dharura wamewasili kwenye eneo la tukio na vituo vya afya katika mkoa huo wanajiandaa kupokea majeruhi.

Klabu ya Chapecoense haijasema lolote. Wachezaji wake wamekua wakisafiri hkjatika mji wa Medellin ili kumenyana na Atletico Nacional katika mechi ya awali ya fainali ya michuano ya Copa Sudamericana.

Ramani ya ajali ya ndege nchini Colombia.
Ramani ya ajali ya ndege nchini Colombia. Véronique Barral/FMM