UEFA-SOKA

Arsenal yapangwa tena na Bayern Munich michuano ya UEFA

Droo ya hatua ya mwondoano kuwania taji la klabu bingwa barani Ulaya UEFA, katika mchezo wa soka imetolewa siku ya Jumatatu.

Matangazo ya kibiashara

Klabu ya Arsenal ya Uingereza kwa kwa mara nyingine imejikuta ikipangwa na Bayern Munich ya Ujerumani kama ilivyokuwa misimu kadhaa iliyopita, sawa na Barcelona ya Uhispania ambayo itapepetana na Paris Saint-Germain ya Ufaransa.

Baada ya kuongoza katika kundi lake, kocha wa Arsenal Arsene Wenger alikuwa anatumai kuwa angeepuka mmoja wa vlabu vikubwa barani Ulaya kwa mara ya kwanza ndani ya miaka mitano lakini historia imejirudia tena.

Beyern ambayo kwa sasa inafunzwa na kocha Carlo Ancelotti, msimu wa mwaka 2012/13, illishinda Arsenal katika hatua hii hali iliyojirudia tena msimu wa 2013/14.

Msimu uliopita, timu hizi mbili zilikutana katika hatua ya makundi.

Mabingwa watetezi Real Madrid ya Uhispania, watamenyana na Napoli ya Italia huku Manchester City ya Uingereza inayofunzwa na Pep Guardiola ikipangwa na Monaco ya Ufaransa.

Michuano hii itachezwa nyumbani na ugenini mwezi Februari na Machi mwaka 2017.

Ratiba kamili:-

  • Manchester City vs Monaco
  • Real Madrid vs Napoli
  • Benfica vs Borrussia Dortmund
  • Bayern Munich vs Arsenal
  • Porto vs Juventus
  • Beyer Leverkusen vs Atletico Madrid
  • Paris Saint-Germain vs Barcelona
  • Sevilla vs Leicester City