SOKA

Cristiano Ronaldo atarajiwa kushinda taji la Ballon d'Or mwaka 2016

Soka
Soka FIFA.COM

Wapenzi wa soka duniani, wanasubiri mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka 2016 maarufu kama Ballon d'Or.

Matangazo ya kibiashara

Mshindi huo atafahamika baadaye siku ya Jumatatu, huku mshambuliaji matata wa klabu ya Real Madrid na raia wa Ureno Cristiano Ronaldo akitarajiwa kunyakua taji hili kwa mara ya tatu.

Ronaldo anapewa nafasi kubwa kwa sababu ameisadia klabu yake kunyakua taji la klabu bingwa barani Ulaya mara mbili kwa misimu mitatu na lilikuwa taji lake la tatu baada ya kuisadia pia Manchester United mwaka 2008.

Mbali na klabu yake, alifanikiwa kuiongoza nchi yake kunyakua taji la bara Ulaya katika michuano iliyofanyika nchini Ufaransa kati ya mwezi Juni na Julai mwaka huu.

Hata hivyo, Ronaldo anakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa mshambuliaji mwenzake kutoka Argetina na mshambuliaji wa Bracelona Lionell Messi, aliyeshinda mwaka 2015.

Washindi wa miaka iliyopita:-

  • 2010-Lionel Messi-Barcelona
  • 2011-Lionel Messi-Barcelona
  • 2012-Lionel Messi-Barcelona
  • 2013-Cristiano Ronaldo-Real Madrid
  • 2014- Cristiano Ronaldo-Real Madrid
  • 2015-Lionel Messi-Barcelona