SOKA-KENYA

Kenneth Muguna ashinda tuzo ya mchezaji mwenye thamani kubwa Kenya

Kiungo wa klabu ya soka ya Western Stima Kenneth Muguna ndio mchezaji  mwenye thamani kubwa mwaka 2016 nchini Kenya.

Kenneth Muguna mshindi wa tuzo ya mchezaji mwenye thamani nchini Kenya mwaka 2016
Kenneth Muguna mshindi wa tuzo ya mchezaji mwenye thamani nchini Kenya mwaka 2016 www.kpl.co.ke
Matangazo ya kibiashara

Kiungo huyo wa Kati, alipata tuzo hiyo siku ya Jumanne usiku wakati wa hafla  jijini Nairobi na kumshinda Eric Ouma wa Gor Mahia na Humfrey Mieno wa Tusker FC.

Licha ya kuwa mchezaji bora, Muguna alipata tuzo ya kiungo bora wa mwaka na kuzawadiwa Shilingi za Kenya Millioni 1.5.

Taji la kocha bora wa mwaka, lilimwendea Paul Nkata wa Tusker FC, baada ya kuiongoza klabu hiyo kushinda taji la msimu huu nchini humo.

Nkata raia wa Uganda, aliwashinda makocha wengine Ze Maria wa Gor Mahia na Francis Baraza kutoka Chemelil Sugar FC.

Orodha Kamili

Kipa bora wa mwaka:
Patrick Matasi – Posta Rangers

Beki bora
Jockins Atudo – Posta Rangers

Kiungo bora wa Kati
Miguna Kenneth – Western Stima

Mfungaji bora
John Makwata – Ulinzi Stars

Mchezaji bora wa mwaka 2016
Eric Ouma – Gor Mahia