CAF-SOKA

Madagascar yaanza vizuri michuano ya ufukweni barani Afrika

Senegal ikimenyana na Morocco katika mchuano wa ufunguzi wa soka la ufukweni nchini Nigeria
Senegal ikimenyana na Morocco katika mchuano wa ufunguzi wa soka la ufukweni nchini Nigeria www.cafonline.com

Timu ya taifa ya soka ya Madgascar ambao ni mabingwa wa soka barani Afrika , wameanza vema harakati za kutetea taji lake baada ya kuishinda Libya mabao 9-5 katika mchuano wa ufunguzi makala ya mwaka huu michuano ya ufukweni inayoendelea  mjini Lagos nchini Nigeria.

Matangazo ya kibiashara

Mabingwa hao ambao wanaongoza kundi la B kwa alama 3 nyuma ya Senegal ambayo pia ilipata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Morocco katika mchuano wa ufunguzi, siku ya Jumatano itamenyana na Senegal.

Mchuano mwingine wa leo, Libya itachuana na Morocco.

Wenyeji Nigeria, nao walianza vema baada ya kuishinda Misri kwa mabao 3-2 huku Ivory Coast ikiishinda Ghana mabao 5-0 katika michuano ya kundi A.

Ratiba ya Jumatano Desemba 14 2016:-

  • Misri vs Ghana
  • Ivory Coast vs Nigeria

Mataifa mawili yatakayofika fainali, yatafuzu katika michuano ya kombe la dunia itakayofanyika nchini Bahamas mwaka ujao.