GHANA-GRANT-AFCON2017

Kocha wa Ghana, Avram Grant ajumuisha wachezaji wanne wapya kwenye kikosi chake

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Ghana, Avram Grant, amewataja wachezaji wanne wapya katika kikosi chake cha awali cha wachezaji 26, tayari kwaajili ya kushiriki michuano ya kombe la mataifa ya Afrika (Total Africa Cup of Nations 2017) itakayofanyika nchini Gabon.

Mshambuliaji André Ayew, akizungumza na kocha mkuu wa Ghana, Avram Grant, 8 Februari 2015 mjini Bata.
Mshambuliaji André Ayew, akizungumza na kocha mkuu wa Ghana, Avram Grant, 8 Februari 2015 mjini Bata. AFP PHOTO / CARL DE SOUZA
Matangazo ya kibiashara

Kwenye orodha yake yumo kiungo, Ebenezer Ofori na Joseph Larweh Attamah, wamo pia washambuliaji, Bernard Tekpetey na Raphael Dwamena.

Ofori anachezea klabu ya Uswisi, AIK, huku mwenzake Attamah yumo katika kikosi cha wachezaji wa timu ya taifa ya Ghana iliyo na umri wa chini ya miaka 20, ambacho kilishinda medali ya fedha katika michuano ya FIFA kombe la dunia iliyofanyika nchini Uturuki mwaka 2013.

Wachezaji hao wanne wameonekana kuwashtua mashabiki wengi wa soka wa Ghana, kuona wamejumuishwa katika kikosi cha Grant, ambacho kinatarajiwa kwenda kupiga kambi katika nchi ya Falme za Kiarabu.

Hakukuwa na nafasi kwa mlinda mlango Fatau Dauda, ambaye hivi karibuni amejiunga na miamba ya Nigeria, Enyimba huku beki wa kushoto wa Leicester City, Jeffery Schlupp akiachwa.

Nahodha Asamoah Gyan anaongoza kikosi hicho, akijiandaa kuichezea timu yake kwa mara ya sita mfululizo katika michuano hii. Wachezaji wengine mashuhuri ni ndugu Andre na Jordan Ayew, wamo pia Emmanuel Agyemang Badu, Christian Atsu na Harrison Afful.

Mabingwa hao mara nne, wamo katika kundi D sambamba na Misri, Mali na Uganda.

Chini ni Kikosi hicho na kwenye mabano ni timu wanazochezea:

Makipa: Razak Braimah (Cordoba, Spain), Adam Kwarasey (Rosenborg, Norway) Richard Ofori (Wa All Stars)

Mabeki: Harrison Afful (Columbus Crew, USA), Andy Yiadom (Barnsley, England), Baba Rahman (Schalke, Germany), Frank Acheampong (Anderlecht, Belgium), John Boye (Sivasspor, Turkey), Jonathan Mensah (Anzhi, Russia), Daniel Amartey (Leicester City, England), Edwin Gyimah (Orlando Pirates, South Africa)

Viungo: Emmanuel Agyemang-Badu (Udinese, Italy), Afriyie Acquah (Torino, Italy), Thomas Partey (Atletico Madrid, Spain), Mubarak Wakaso (Panathinaikos, Greece), Christian Atsu (Newcastle, England), Ebenezer Ofori (AIK Stockholm, Sweden), Samuel Tetteh (Leifering, Austria), Joseph Larweh Attamah (Başakşehir F.K, Turkey)

Washambuliaji: Asamoah Gyan (Al Ahli, UAE), Jordan Ayew (Aston Villa, England), Abdul-Majeed Waris (Lorient, France), Andre Ayew (West Ham, England), Ebenezer Assifuah (Sion, Switzerland), Bernard Tekpetey (Schalke, Germany), Rahpael Dwamena (Austria Lustenau, Austria)