MPIRA WA MIGUU-CHAPECOENSE

Klabu ya Chapecoense kusajili wachezaji 20 kujiandaa na msimu mpya wa ligi

Nembo ya klabu ya Chapecoense.
Nembo ya klabu ya Chapecoense. http://www.chapecoense.com/2016/img/banners/

Klabu ya mpira wa miguu nchini Brazil ya Chapecoense, itafanya usajili wa wachezaji wapya 20 kwaajili ya msimu ujao wa ligi kuu, ambapo namba za wachezaji walionusurika katika ajali ya ndege zitahifadhiwa.

Matangazo ya kibiashara

Wachezaji 19 na benchi la ufundi la timu hiyo, walikufa katika ajali ya ndege mwezi Novemba mwaka jana, wakati ndege waliyokuwa wakitumia kusafiria, kuanguka wakati ikielekea Colombia kucheza mchezo wa fainali ya kombe la Copa Sudamericana.

Timu hiyo ilipewa kombe la fainali hiyo, huku wapinzani waliokuwa wacheze nao klabu ya Atletico Nacional, wakipewa tuzo ya Fair Play.

"Mkurugenzi wa ufundi wa timu hiyo, Rui Costa, amesema kuwa "sasa tunajaribu kupata mikopo."

Beki wa kati wa timu hiyo, Neto na beki wa kulia Alan Ruschel walinusurika katika ajali hiyo na Costa anasema "tunatarajia wachezaji hawa wawili kurejea uwanjani na kuvaa jezi zao".

Mlinda mlango wa akiba wa timu hiyo Jackson Follmann alinusurika kwenye ajali hiyo lakini akalazimika kukatwa mguu wake.

"Hakuna mchezaji ambaye atavaa namba za jezo zilizokuwa zinatumiwa na Alan pamoja na Neto wala Follmann.

Chapecoense, ambayo itaanza mazoezi ya msimu mpya Ijumaa ya wiki hii, itacheza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Joinville Januari 26.