TUZO MCHEZAJI BORA AFRIKA-CAF

Mchezaji bora wa Afrika kujulikana Januari 5

Nembo ya CAf inayotumiwa katika tuzo za mchezaji bora barani Afrika
Nembo ya CAf inayotumiwa katika tuzo za mchezaji bora barani Afrika Cafonline.com

Tuzo za mwaka za shirikisho la kabumbu barani Afrika CAF, zinaingia katika makala yake ya 25 na sherehe za utoaji wa tuzo ya mchezaji bora barani Afrika zitafanyika kwa mara ya pili mfululizo kwenye jiji kuu la Nigeria, Abuja. 

Matangazo ya kibiashara

Alhamisi ya tarehe 5 Januari, 2017, mfalme wa soka barani Afrika atapewa tuzo yake katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa jijini Abuja, ambapo miongoni mwa wanaowania tuzo hiyo, ni pamoja na Pierre-Emerick Aubameyang wa Gabon ambaye mwaka jana alikuwa kwenye orodha pia ya wanaowania tuzo hii.

Yumo Riyad Mahrez wa Algeria anayekipiga na klabu ya Leicester City ya Uingereza pamoja na mshambuliaji wa kimataifa wa Senegal, Sadio Mane anayekipiga na klabu ya Liverpool ya Uingereza.

Kuanzia mwaka 1992 hadi mwaka 2015, kuanzia kwa Mghana Abedi Pele hadi kwa Mgabon Aubameyang, wachezaji 15 wamefanikiwa kutwaa tuzo ya mchezaji bora barani Afrika na tuzo nyingine za dunia.

Aliyekuwa nahodha wa Cameroon, Samuel Eto'o alikuwa mchezaji wa kwanza kushinda tuzo hiyo mara nne ambapo alishinda mwaka 2003, 2004, 2005 na 2010, rekodi ambayo ilifikiwa pia na kiungo wa Ivory Coast Yaya Toure aliyeshinda mwaka 2011, 2012, 2013 na 2014.

Mchezaji mwingine aliyewahi shinda tuzo hiyo ni aliyekuwa mshambuliaji wa Senegal El Hadji Diouf aliyeshinda taji hili mara mbili, mwaka 2001 na 2002.

Hata hivyo mchezaji wa kwanza kuwahi kushinda taji hili la CAF mara mbili, alikuwa ni nahodha wa dhamani wa Nigeria, Nwanko Kanu aliyeshinda mwaka 1996 na 1999, kabla ya Didier Drogba kushinda mwaka 2006 na 2009.

Washindi wa taji la mchezaji bora barani Afrika wengine wanacheza ama nafasi ya kiungo au ushambuliaji, na utamaduni huu huenda ukarejelewa tena mwaka huu kutokana na wachezaji waliomo kwenye orodha hiyo, ambapo wachezaji wote watatu ni washambuliaji.

Ifuatayo ni orodha ya wachezaji waliowahi kushinda tuzo hii:

1992 Abedi AYEW PELE (Ghana)
1993 Rashidi YEKINI (Nigeria)
1994 Emmanuel AMUNIKE (Nigeria)
1995 George WEAH (Liberia)
1996 Nwankwo KANU (Nigeria)
1997 Victor IKPEBA (Nigeria)
1998 Mustapha HADJI (Morocco)
1999 Nwankwo KANU (Nigeria)
2000 Patrick MBOMA (Cameroon)
2001 El-Hadji DIOUF (Senegal)
2002 El Hadji DIOUF (Senegal)
2003 Samuel ETO'O (Cameroon)
2004 Samuel ETO'O (Cameroon)
2005 Samuel ETO'O (Cameroon)
2006 Didier DROGBA (Côte d’Ivoire)
2007 Frederic KANOUTE (Mali)
2008 Emmanuel ADEBAYOR (Togo)
2009 Didier DROGBA (Côte d’Ivoire)
2010 Samuel ETO'O (Cameroon)
2011 Yaya TOURE (Côte d’Ivoire)
2012 Yaya TOURE (Côte d’Ivoire)
2013 Yaya TOURE (Côte d’Ivoire)
2014 Yaya TOURE (Côte d’Ivoire)
2015 Pierre-Emerick AUBAMEYANG (Gabon)
2016 ?????