Serena atupwa nje michuano ya Auckland, New Zealand
Imechapishwa:
Mchezaji nambari mbili kwa ubora wa mchezo wa tenesi duniani upande wa wanawake, Serena Williams, amepoteza mchezo wake wa raundi ya pili ya ASB mjini Auckland New Zealand.
Akirejea kutoka kwenye majeraha ya bega na goti, Serena alipoteza mchezo wake dhidi ya Madison Brengle kwa seti 4-6, 7-6 na 4-6.
Williams amerejea uwanjani baada ya kuwa nje ya uwanja kwa miezi minne, akidai kuwa bado hajarejea kwenye kiwango chake cha awali.
Ilikuwa ni siku mbaya kwa wanandugu Serena na Venus, ambao wameshuhudia wote wakitupwa nje, ambapo Venus alijikuta akiamua kujiondoa kwenye mchezo wake baada ya kupata jeraha la bega.
Mkurugenzi wa mashindano haya, Karl Budge, amesema kuwa bingwa mara saba wa Grand Slams, alishindwa kuendelea na mchezo baada ya kugundua kuwa alipata jeraha kwenye bega.