CAF-MISRI

Rais wa CAF, Issa Hayatou kuchunguzwa na mamlaka nchini Misri kwa ubadhirifu

Issa Hayatou, rais wa shirikisho la soka barani Afrika, CAF.
Issa Hayatou, rais wa shirikisho la soka barani Afrika, CAF. FABRICE COFFRINI / AFP

Mamlaka nchini Misri zimesema kuwa zimepeleka shauri la tuhuma za matumizi mabaya ya ofisi dhidi ya rais wa Shirikisho la mpira wa miguu barani Afrika, CAF, Issa Hayatou kwa mwendesha mashtaka wa Serikali.

Matangazo ya kibiashara

Tuhuma dhidi ya Hayatou zinahusiana na namna ambavyo kiongozi huyo alitoa haki za televisheni kwa kampuni ya michezo ya Lagardere haki ya kuonesha michuano kadhaa inayosimamiwa na shirikisho hili.

Kwa mujibu wa sheria za ushindani za mamlaka ya ushindani nchini Misri, Issa Hayatou anatuhumiwa kwa kushindwa kuweka wazi kwa uma, tenda huru na wazi kwa makampuni mengine ya habari kushindana kama inavyotakiwa na sheria za Misri.

Ofisi za shirikisho la kabumbu barani Afrika CAF ziko jijini Cairo Misri na mamlaka nchini humo zinasema kuwa ni lazima shirikisho hilo lifuate sheria za nchi hiyo.

Hata hivyo shirikishi hilo bado halijatoa kauli yoyote wala Issa Hayatou mwenyewe hakupatikana kuweza kulizungumzia.

Tayari kampuni ya Lagardere imekanusha tuhuma hizi ikisema kuwa ni tuhuma zisizo na msingi wowote.