TUZO CAF 2016

Tuzo za CAF 2016: Aubameyang, Mehrez na Mane nani kuwa mchezaji bora wa Afrika

Mchezaji bora wa Afrika kwa mwaka 2016 hatimaye atajulikana hii leo, wakati wa sherehe za utoaji wa tuzo mbalimbali, sherehe zinazofanyika kwa mara ya pili mfululizo jijini Abuja, Nigeria.

Nembo ya CAf inayotumiwa katika tuzo za mchezaji bora barani Afrika
Nembo ya CAf inayotumiwa katika tuzo za mchezaji bora barani Afrika Cafonline.com
Matangazo ya kibiashara

Waandaji wa tuzo hizi tayari wamethibitisha kuwa washereheshaji wa tuzo hizi watakuwa ni mwanadada Mimi Fawaz, anayetangaza kwenye kipindi cha michezo cha 360 kinachorushwa kwenye chaneli ya Vox Africa akisaidiana na muigizaji mkongwe nchini Nigeria, Richard Mofe-Damijo.

Ifuatayo ni orodha ya tuzo zitakazoshindaniwa:

Wanaowania tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika:

Pierre-Emerick AUBAMEYANG (Gabon & Borussia Dortmund)
Riyad MAHREZ (Algeria & Leicester City)
Sadio MANE (Senegal & Liverpool)

Wanaowania tuzo Mchezaji Bora wa Afrika anayecheza ligi za Afrika:

Denis ONYANGO (Uganda & Mamelodi Sundowns)
Khama BILLIAT (Zimbabwe & Mamelodi Sundowns)
Rainford KALABA (Zambia & TP Mazembe)

Wanaowania tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika kwa wanawake:

Asisat OSHOALA (Nigeria & Arsenal Ladies)
Elizabeth ADDO (Ghana & Kvarnsvedensik)
Gabrielle ABOUDI ONGUENE (Cameroon & Rossyanka)

Wachezaji wanaowania tuzo wa mchezaji Chipukizi:

Elia MESCHAK (DR Congo & TP Mazembe)
Kelechi IHEANACHO (Nigeria & Manchester City)
Naby KEITA (Guinea & RB Leipzig)

Wachezaji wanaowania tuzo ya Mchezaji Bora Kijana:

Alex IWOBI (Nigeria and Arsenal)
Eric AYIAH (Ghana and Charity FC)
Sandra OWUSU-ANSAH (Ghana and Supreme Ladies)

Wanaowania Tuzo ya Kocha Bora wa Mwaka:

Florent IBENGE (DR Congo national team)
Pitso MOSIMANE (Mamelodi Sundowns)
Florence OMAGBEMI (Nigeria women’s national team)

Timu zinazowania tuzo ya klabu Bora ya Mwaka:

Mamelodi Sundowns
TP Mazembe
Zesco United

Timu za taifa zinazowania tuzo ya timu ya taifa Bora ya Mwaka:

DR Congo
Senegal
Uganda

Wanaowania tuzo ya timu bora ya Taifa ya wanawake ya Mwaka:

Cameroon
Nigeria
South Africa

Waamuzi wanaowania tuzo ya Refa Bora wa Mwaka:

Bakary Papa GASSAMA
Ghead Zaglol GRISHA
Malang DIEDHIOU

Anayewania tuzo ya Kiongozi Bora wa Mwaka wa mpira wa Miguu:

Manuel LOPES NASCIMENTO, Rais wa shirikisho la soka nchini Guinea Bissau

Wanaowania tuzo ya Mchezaji aliyepata mafanikio:

Laurent POKOU, Former player of Cote d’Ivoire
Emilienne MBANGO, Former player of Cameroon

Kikosi cha Kwanza cha Afrika:

Mlinda Mlango: Denis ONYANGO (Uganda & Mamelodi Sundowns).

Walinzi: Serge AURIER (Cote d’Ivoire & Paris Saint-Germain), Aymen ABDENNOUR (Tunisia & Valencia), Eric BAILLY (Cote d’Ivoire & Manchester United), Joyce LOMALISA (DR Congo & AS Vita).

Viungo: Khama BILLIAT (Zimbabwe & Mamelodi Sundowns), Rainford KALABA (Zambia & TP Mazembe), Keegan DOLLY (South Africa & Mamelodi Sundowns).

Washambuliaji: Pierre-Emerick AUBAMEYANG (Gabon & Borussia Dortmund), Sadio MANE (Senegal & Liverpool), Riyad MAHREZ (Algeria & Leicester City)

Wachezaji wa Akiba:

Aymen MATHLOUTHI (Tunisia & Etoile du Sahel), Kalidou KOULIBALY (Senegal & Napoli), Salif COULIBALY (Mali & TP Mazembe), Islam SLIMANI (Algeria & Leicester City), Mohamed Salah (Egypt & Roma), Kelechi IHEANACHO (Nigeria & Manchester City), Alex IWOBI (Nigeria and Arsenal)