Ufaransa ilipata Euro Bilioni 1.2 wakati ya michuano ya Euro 2016
Imechapishwa:
Wizara ya Michezo nchini Ufaransa imetangaza kuwa ilitumia Euro Milioni 200 kuandaa michuano ya soka ya Euro kuwania taji la bara Ulaya mwaka 2016, na kupata faida ya Euro Bilioni 1 nukta 2.
Tangazo hili limetolewa baada ya kuwepo kwa malalamishi ya raia wa Ufaransa kwa kutumia fedha nyingi kuandaa michuano hiyo badala ya kutumia fedha hizo kukabiliana na ugaidi.
Ufaransa imesema fedha, zilipatikana kutokana na idadi kubwa ya watalii waliotembelea nchi hiyo wakati wa michuano hiyo.
Shirikisho la soka barani Ulaya UEFA, lilitumia Euro Milioni 360 kusaidia Ufaransa kufanikisha mashindano hayo.
Mataifa 24 yalishiriki katika michuano, ambayo Ureno ilishinda baada ya kuifunga Ufaransa bao 1-0 katika mchuano wa fainali uliochezwa katika uwanja wa Saint-Denis jijini Paris.