AFCON 2017

Vlabu vya Uingereza vitakavyosa wachezaji muhimu wakati wa michuano ya AFCON

Nembo ya Shirikisho la soka barani Afrika CAF
Nembo ya Shirikisho la soka barani Afrika CAF cafoline

Kuelekea katika michuano ya mataifa bingwa barani Afrika siku ya Jumamosi nchini Gabon, klabu ya Leicester City nchini Uingereza na Stoke City, itawakosa wachezaji wao muhimu baada ya kurudi nyumbani kuzisaidia nchi zao.

Matangazo ya kibiashara

Vlabu vingine ambavyo pia vitakosa huduma za wachezaji wao ni pamoja na Liverpool na Manchester United.

Leicester City itakosa huduma za wachezaji watatu wa kutegemewa ambao ni pamoja na Riyad Mahrez, Islam Slimani na Daniel Amartey ambao ni tegemeo kubwa kwa klabu yao.

Manchester United itakosa huduma za mchezaji Eric Bailly ambaye amerudi nyumbani kuichezea Ivory Coast huku Sadio Mane wa Liverpool, akirudi nyumbani kwenda kuichezea Senegal.

Arsenal, nayo itakosa huduma za mchezaji wa Misri Mohamed Elneny.

Klabu ya Stoke City nayo itawakosa wachezaji watatu, Wilfried Bony (Ivory Coast), Ramadan Sobhi (Misri ) na Mame Biram Diouf (Senegal).

West Ham United nayo itavumilia ukosefu wa wachezaji wa Cheikhou Kouyate (Senegal) na Andre Ayew (Ghana).