FIFA

Kenya yapanda nafasi mbili viwango vya mchezo wa soka duniani

Timu ya taifa ya soka ya Kenya, Harambee Stars.
Timu ya taifa ya soka ya Kenya, Harambee Stars. youtube

Kenya imepanda nafasi mbili katika orodha ya mwezi Januari kuonesha viwango vya mchezo wa soka duniani, inayotolewa na Shirikisho la soka FIFA.

Matangazo ya kibiashara

Harambee Stars ya Kenya ambayo ilikuwa na 89 mwezi uliopita, sasa ni ya 87.

Uganda ambayo imekuwa ikiongoza katika ukanda wa Afrika Mashariki, imeshuka nafasi moja na sasa ni ya 73 lakini inasalia nchi bora katika ukanda wa CECAFA.

Cranes ambayo inashiriki katika michuano ya mataifa bingwa barani Afrika nchini Gabon, siku ya Jumanne ilifungwa na Ivory Coast mabao 3-0 katika mchuano wa Kimataifa wa kujipima nguvu.

DR Congo ni ya sita barani Afrika. Tanzania ya 49 barani Afrika na ya 156 duniani.

Rwanda nayo imeshuka hadi katika nafasi ya 93 huku Ethiopia ikiwa ya 112.

Sudan na Burundi zimeshuka nafasi mbili. Sudan ni ya 217 duniani huku Burundi ikiwa ya 139.

Senegal ndio taifa bora barani Afrika, ikifuatwa na Ivory Coast, Misri na Tunisia.

Argetina inaongoza duniani, ikifuatwa na Brazil, Ujerumani , Chile huku Ubelgji ikifunga tano bora.