AFCON 2017-GABON-Burkina Faso

Afcon 2017: Gabon na Burkina Faso zatoka sare ya kufungana 1-1

Pierre-Emerick Aubameyang, mshambuliaji wa Gabon, akifanyiwa madhambi na Hervé Koffi,kipa wa Burkina Faso wakati wa mchezo kati ya Gabon na Burkina Faso, Januari 18, 2017 kwenye uwanja wa Amitié.
Pierre-Emerick Aubameyang, mshambuliaji wa Gabon, akifanyiwa madhambi na Hervé Koffi,kipa wa Burkina Faso wakati wa mchezo kati ya Gabon na Burkina Faso, Januari 18, 2017 kwenye uwanja wa Amitié. RFI/Pierre René-Worms

Mechi za mchezo wa soka mzunguko wa pili hatua ya makundi kutafuta ubingwa wa bara Afrika, zilianza kuchezwa Jumatano hii nchini Gabon.

Matangazo ya kibiashara

Wenyeji Gabon walirejea tena katika uwanja wa Amitie, jijini Libreville, kumenyana na Burkina Faso. Lakini hadi mchezo kumalizika timu hizo zilijikuta zikitoka sare ya kufungana 1-1.

Gabon na Burkina Faso walicheza mchezo wao wa pili baada ya mechi zao za kwanza zilizomalizika kwa sare ambapo Gabon ilitoka sare dhidi ya Guinea Bissau na Burkina Faso ikitoka sare dhidi ya Cameroon

Burkina Faso ndio ilianza kuliona lango la Gabon katika kipindi cha kwanza cha mchezo.

Pierre-Emerick Aubameyang alifunga bao la kusawazisha kupitia mkwaju wa penalti baada ya bao la Burkina Faso katika kipindi cha kwanza.

Mechi hii ilichezwa kuanzia saa moja kamili jioni saa za Afrika Mashariki, chini ya refarii kutoka Gambia Bakary Gasssama.

Gabon ilikua inatumai kuwa itaandikisha ushindi, ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kufuzu katika mzunguko wa pili na kuwafurahisha mashabiki wa nyumbani.

Hadi sasa, ni mataifa matatu kati ya 16 yanayoshiriki katika michuano hii ambayo yamepata ushindi katika mzunguko wa kwanza.