AFCON 2017-GABON

Wenyeji Gabon na Guinea-Bissau watupwa nje michuano ya AFCON 2017

Timu ya taifa ya Gabon imekuwa ni taifa la pili ambaye ni mwenyeji wa michuano ya kombe la mataifa ya Afrika, kuaga michuano ya mwaka huu kwenye hatua ya makundi, baada ya kulazimishwa sare na timu ya taifa ya Cameroon, mjini Libreville, siku ya Jumapili ya Januari 22.

Kipa wa Cameroon Ebogo Ondoa akipangua shuti la mpira wa faulo uliopigwa na mchezaji wa Gabon. Januari 22, 2017
Kipa wa Cameroon Ebogo Ondoa akipangua shuti la mpira wa faulo uliopigwa na mchezaji wa Gabon. Januari 22, 2017 ©Pierre René-Worms
Matangazo ya kibiashara

Nahodha wa timu ya taifa ya Gabon, Pierre-Emerick Aubameyang, aliikosesha nafasi ya wazi timu yake kutinga kwenye hatua ya robo fainali ya michuano ya mwaka huu, baada ya kukosa goli la wazi kabisa katika dakika za wali za kipindi cha kwanza.

Mchezaji mwenzake, Denis Bouanga, alijikuta akiangua kilio mara baada ya mechi, kufuatia mpira wa dakika za lala salama kugonga mwamba na kushindwa kuipa ushindi timu yake.

Licha ya kumaliza hatua ya makundi ikiwa haijapoteza mechi hata moja, Gabon imekuwa taifa la nne na la kwanza kutolewa toka ilipokuwa hivyo kwa timu ya taifa ya Tunisia mwaka 1994 ambao nayo iliondolewa kwenye hatua ya makundi.

Wachezaji wa Gabon wakiwania mpira mbele ya mchezaji wa Cameroon, wakati wa mchezo wao wa siku ya Jumapili, Januari 22.
Wachezaji wa Gabon wakiwania mpira mbele ya mchezaji wa Cameroon, wakati wa mchezo wao wa siku ya Jumapili, Januari 22. ©Pierre René-Worms

Katika hatua nyingine, timu ya taifa ya Cameroon licha ya kukabiliwa na baadhi ya wachezaji wake kuikacha timu hiyo, imetinga kwenye hatua ya nane bora kwa kumaliza katika nafasi ya pili kwenye kundi A.

Timu ya taifa ya Burkina Faso, yenyewe imemaliza ya kwanza kwenye kundi A, baada ya kufanikiwa kuchomoza na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya timu ngeni kwenye michuano ya mwaka huu, Guinea Bissau.

Aubameyang aliifungia timu yake bao katika kila mechi mbili za ufunguzi, na walifanikiwa kumaliza kwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Guinea-Bissau na Burkina Faso.

Mchezaji wa Gabon, Bouanga ndiye aliyekuwa mchezaji kinara kwa timu yake, na alifanya kila linalowezekana kuitafutia timu yake bao, huku mpira alioupiga kwenye dakika ya 94 ya mchezo ukogonga mwamba na kurejea uwanjani>

Wakati wachezaji wa Gabon wakiangua kilio, kocha mkuu wa timu hiyo, Jose Antonio Camacho alikataa kuingizwa kwenye mjadala wa kuhusu hatma yake kama kocha mkuu wa Gabon, badala yake akaomba radhi kwa mashabiki kutokana na timu yao kutolewa huku akisema bahati haikuwa yao.

Timu nyingine zilizoaga michuano ya mwaka huu ya Gabon ni, Uganda, Guinea-Bissau na wenyeji Gabon.

Mechi nyingine zitapigwa Jumanne ya tarehe 23, ambapo Zimbabwe watacheza na Tunisia, huku Senegal ambao wameshakata tiketi wao watacheza na Algeria, kwenye mchezo utakaopigwa kwenye dimba la "Stade d'Angondje" majira ya saa nne kamili usiku kwa saa za Afrika Mashariki.