AFCON 2017

Uganda kujaribu kupata ushindi kabla ya kurejea nyumbani

Mchuano uliopita kati ya Uganda na Misri
Mchuano uliopita kati ya Uganda na Misri Pierre-René Worms - RFI

Michuano ya soka hatua ya makundi kutafuta taji la AFCON mwaka 2017 inamalizika siku ya Jumatano usiku nchini Gabon.

Matangazo ya kibiashara

Timu katika kundi D, zinajitosa uwanjani mjini Port-Gentil na Oyem kunzia saa nne usiku saa za Afrika Mashariki.

Mchuano wa leo ni muhimu sana kwa Misri na Mali ambazo zote zinatafuta kufuzu katika hatua ya robo fainali.

Hadi sasa Ghana imeshafuzu katika hatua hiyo baada ya kupata ushindi katika michuano miwili iliyopita.

Black Stars iliishinda Uganda bao 1-0 lakini pia ikapata ushindi kama huo dhidi ya Mali.

Ghana leo inamenyana na Misri mjini Port Gentil, mchuano ambao mwamuzi wa kati atakuwa ni Bakary Gassama kutoka Gambia.

Misri inahitaji sare ili kusonga mbele lakini hata ikifungwa na Ghana, iombe Uganda iifunge Mali ambayo hadi sasa ina alama moja.

Mali ambayo inacheza na Uganda, inaweza kufuzu ikiwa itashinda mechi ya leo kwa mabao mengi lakini pia kuomba kuwa Ghana iwafunge Misri.

Mchuano kati ya Mali na Uganda utachezwa katika uwanja wa Oyem.

Uganda imeshaondolewa katika michuano hii baada ya kufungwa michuano yake miwili dhidi ya Ghana na Misri kwa bao 1-0.

Ratiba ya robo fainali

Januari 28 2017
Burkina Faso vs Tunisia
Senegal vs Camroon

Januari 29 2017
DR Congo vs Mshindi wa pili wa kundi D
Morocco vs Mshindi wa kundi D