AFCON 2017-GABON-BURKINA FASO-MISRI

AFCON 2017: Misri yatinga fainali, baada ya miaka saba

Mchuano wa kwanza wa nusu fainali katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON 2017 umepigwa Jumatano hii Februari 1 kwenye uwanja wa Amitie nchini Gabon, kati ya Burkina Faso na Misri.

Essam El-Hadary (kushoto), kipa wa Misri, aonekana kiungo muhimu katika mchuano kati ya timu yake na Burkina Faso na kupelekea ushindi wa timu yake.
Essam El-Hadary (kushoto), kipa wa Misri, aonekana kiungo muhimu katika mchuano kati ya timu yake na Burkina Faso na kupelekea ushindi wa timu yake. RFI/Pierre René-Worms
Matangazo ya kibiashara

Watu karibu 19,422 walikua uwanjani wakitazama pambano hilo. Hadi dakika ya 120, timu zote mbili zilijikuta zikiingia katika hatua ya mikwaju ya penalti. Hata hivyo Misri waliibuka mshindi kwa kuingiza mikwaju 4 dhidi ya 3 ya Burkina Faso, baada ya kutoka sare ya kufungana 1-1.

Misri na Burkina Faso walimenyana katika nusu fainali miaka 19 iliopita katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika tarehe 25 Februari 1998 nchini Burkina faso. Wakati huo Burkina Faso ilifungwa na Misri kwa mabo 2-0. Wakati huo huo Misri pia waliibuka msindi kwa kuwafunga Afrika Kusini katika fainali kwa mabao 2-0.

Misri na Burkina Faso wamlionyesha mchezo mzuri, licha ya kuwa kila timu ilikiwa ikitawala mpira kwa muda wa dakika fulani.