AFCON 2017-GABON-CAMEROON-MISRI

Cameroon yashinda Kombe la Mataifa ya Afrika 2017 kwa kuifunga Misri 2-1

Filimbi ya mwisho! Cameroon washinda Kombe la tano la Mataifa ya Afrika.
Filimbi ya mwisho! Cameroon washinda Kombe la tano la Mataifa ya Afrika. RFI/Pierre René-Worms

Cameroon imeshinda taji la mabingwa wa Afrika Jumapili Februari 5 mjini Libreville kwa kuwafunga Misri 2-1 katika fainali ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika. Simba wa Nyika wa Cameroon ambao wamekua wamesha shindia Kombe hilo mara nne walipata ushindi dhidi ya Misri kupitia mchezaji Vincent Aboubakar.

Matangazo ya kibiashara

Misri ndi walianza kuliona lango la Cameroon, lakini hadi mchezo huo kumalizika Mirsi walijikuta wakiburuzwa mabado 2-1.

Itakumbukwa kwamba Misi tayari wameshatwaa Kombe la Mataifa ya Afrika mara saba. Simba wa Nyika wamewashangaza wengi kwa kupata ushindi huo, lakini ndio hivyo hakuna mtaalamu kwa kabumbu.

Vincent Aboubakar akionyesha ujuzi wake.
Vincent Aboubakar akionyesha ujuzi wake. RFI/Pierre René-Worms

Simba wa Nyika walikua na bahati nzuri ya kufika katika fainali baada ya kuwabwaga Senegal kwa mshangao mkubwa katika robo fainali na kumuangusha Ghana katika nusu fainali. Na sasa Misri walikua chakula cha mwisho Simba wa Nyika kwa kufunga mabao 2-1. Tulipata nguvu zaidi kwa kuwa na wachezaji Nicolas Nkoulou na Vincent Aboubakar, na hapo inaonyesha jinsi gani tuko kitu kimoja, " amesema Georges Mandjeck.

"Si wachezaji 23 ambao walishinda taji hili, lakini marafiki 23," kocha Hugo Broos, kutoka Ubelgiji, amesema. Awali, kocha alikua na imani ya kufanikiwa tu kuingia katika mzunguko wa kwanza. "Tulianza kupata matumani ya kusonga mbele baada ya kuwabwaga, " ameongeza Hugo Broos.

"Pamoja na Kombe la Dunia nchini Mexico mwaka 1986, tulipochukua nafasi yanne na taji la Gabon, nina amini kuwa bado nina uzoefu na nguvu," amesema kocha wa zamani wa FC Bruges. Lakini hapendelei serikali y Cameroon kujega sanamu kwa niaba yake. "Baada ya miaka 42 katika soka, najua vizuri sana kwamba leo mimi sasa ni mfalme, lakini kesho ninaweza kuuawa, kwa hiyo bado kuna kazi kubwa ya kufanya kwa Simba wa Nyika, ambao watalazimika kutetea taji hili mwaka 2019 wakiwa nyumbani, " amesema kocha wa Cameroon.

Timu ya Cameroon wamekusanyika karibu na Kombe walilonyakua baada ya kuwashinda Msri 2-1.
Timu ya Cameroon wamekusanyika karibu na Kombe walilonyakua baada ya kuwashinda Msri 2-1. RFI/Pierre René-Worms