Pata taarifa kuu
SOKA

Christian Bassogog asajiliwa na klabu ya Henan Jianye nchini China

Christian Bassogog (Katikati) akipambana na wachezaji wa Misri wakati wa michuano ya AFCON 2017
Christian Bassogog (Katikati) akipambana na wachezaji wa Misri wakati wa michuano ya AFCON 2017 RFI/Pierre René-Worms
Ujumbe kutoka: Victor Melkizedeck Abuso
Dakika 1

Christian Bassogog mchezaji wa timu ya taifa ya Cameroon, ameungana na klabu ya Henan Jianye nchini China, akitokea klabu ya Aab Fodbold ya Denmark.

Matangazo ya kibiashara

Kiungo huyo wa kati alifanya vizuri wakati wa michuano ya mataifa bingwa barani Afrika nchini Gabon mapema mwezi huu na kuisaidia nchi yake kunyakua taji hilo la AFCON.

Bassogog mwenye umri wa miaka 21, alitajwa kuwa mchezaji bora katika michuano hiyo kutokana namna alivyocheza na kuisaidia nchi yake kupeleka kombe nyumbani.

Mchezeaji huyo amesema amepata makaribisho mazuri kutoka kwa klabu hiyo mpya, na asingeweza kukataa nafasi hiyo baada ya kusajiliwa kwa kima cha Dola za Marekani Milioni 8.7.

Bassogog sasa anaungana na wachezaji wengine kutoka barani Afrika ambao wamekwenda kucheza soka nchini China kama John Mikel Obi na Odion Ighalo wote kutoka nchini Nigeria.

Stephane M’Bia pia kutoka Cameroon anachezea klabu ya Hebei CFFC nchini China.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.