GHANA

shirikisho la mpira Ghana lamteua Maxwell Konadu kuwa kocha wa muda

Aliyekuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Ghana, Avrant Grant.
Aliyekuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Ghana, Avrant Grant. ISSOUF SANOGO / AFP

Shirikisho la soka nchini Ghana, limemrejesha kocha mzawa Maxwell Konadu, kuwa kocha mkuu wa muda wa kikosi cha timu ya taifa, hadi pale shirikisho litakapomtangaza kocha atakayechukua nafasi ya Avrant Grant.

Matangazo ya kibiashara

Konadu, mwenye umri wa miaka 44, aliwahi kushikilia nafasi hiyo mwaka 2014 baada ya aliyekuwa kocha mkuu wakati huo Kwesi Appiah kuondoka, Konadu amekuwa pia kocha wa timu ya vijana chini ya umri wa miaka 20 na 23.

Mabadiliko haya yametangazwa juma hili ambapo pia wamemtangaza Profesa Joseph Mintah kama kocha msaidizi.

Mintaha hata hivyo ataendelea kushikiliza nafasi yake ya awali ambapo alikuwa ni mshauri na mtaalamu wa masuala ya Saikolojia wa timu ya taifa.

Uamuzi huu umekuja baada ya aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo, Muisrael Avrant Grant kuachia nafasi yake baada ya kumalizika kwa michuano ya kombe la mataifa ya Afrika nchini Gabon mwaka huu (2017).

Grant aliiongoza timu hiyo kumaliza kwenye nafasi ya ne ya michuano ya mwaka huu.