LA LIGA

Baada ya kupata majeraha ya kichwa mchezaji Fernando Torres aruhusiwa kutoka hospitali

Madaktari na watoa huduma ya kwanza wakiwa wamembeba kwenye machela mchezaji wa klabu ya Atletico Madrid, Fernando Torres. 2 Machi 2017.
Madaktari na watoa huduma ya kwanza wakiwa wamembeba kwenye machela mchezaji wa klabu ya Atletico Madrid, Fernando Torres. 2 Machi 2017. REUTERS/Miguel Vidal

Mshambuliaji wa klabu ya Atletico Madrid ya Uhispania, Fernando Torres, amefanyiwa vipimo vya kichwa na kutuhusiwa kutoka hospitalini alikokimbizwa baada ya kugongana na mchezahi wa klabu ya Deportivo La Coruna, kwenye mchezo wa ligi kuu ya nchi hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Torres mwenye umri wa miaka 32 alitumia usiku mzima hospitalini baada ya kuanguka vibaya kutokana na kugongwa kichwani wakati akiwania mpira na mchezaji Alex Bergantinos, katika mchezo uliomalizika kwa sare ya bao 1-1.

Klabu ya Atletico Madrid imethibitisha kutoka hospitalini kwa mchezaji huyo, ambapo imesema madaktari wamemtaka apumzike kwa saa 48, licha ya kuwa hakupata majeraha yoyote yaliyohatarisha ubongo wake.

Akitoka hospitalini, Torres amesema anwashukuru wale wote waliomuhudimia na kumuombea na kwamba kilichotokea ilikuwa ni uwoga na sasa anaendelea vizuri.

Baada ya mchezaji huyu wa zamani wa Liverpool na Chelsea kuumia katika dakika ya 85 ya mchezo dhidi ya La Coruna, wachezaji kutoka timu zote mbili waliwahi kumuhudumia na kuwaita madaktari haraka.

Mchezaji huyu alihudumiwa kwa dakika kadhaa ndani ya uwanja na madaktari, kabla ya kutolewa nje kwa machela na kisha kukimbizwa hospitali.