MEXICO OPEN

Tenesi: Djokovic atupwa nje michuano ya Mexico Open

Mchezaji tenesi nambari 2 kwa ubora duniani, Novak Djokovic.
Mchezaji tenesi nambari 2 kwa ubora duniani, Novak Djokovic. Reuters/Henry Romero

Mchezaji nambari mbili kwa ubora wa mchezo wa tenesi duniani, Novak Djokovic, ametupwa nje ya michuano ya Mexico Open katika mchezo wa robo fainali ya michuano hiyo kwa seti mbili bila na mchezaji Nick Kyrgios.

Matangazo ya kibiashara

Mserbia Djokovi ameangukia pua kwa matokeo ya seti 7-6 na 7-5, katika mchezo uliodumu kwa muda wa saa moja na dakika 47, mchezo ambao ulikuwa ni wa kwanza kwa wachezaji hao wawili kukutana,

Djokovic mwenye umri wa miaka 29, alikuwa amerejea kwenye michuano ya Acapulco juma hili ikiwa ni mara ya kwanza toka alipotolewa kwenye mzunguko wa pili wa michuano ya Australian Open mwezi Januari mwaka huu.

Kyrgios mwenye umri wa miaka 21 baada ya kuchomoza na ushindi huu, sasa atakutana na Mmarekani Sam Querrey siku ya Ijumaa.

Katika hatua nyingine mchezaji Rafael Nadal pamoja na Mcroatia Marin Cilic watakutana katika mchezo mwingine wa hatua ya nusu fainali.