EPL-CHELSEA

Conte awataka wachezaji wake kuwa makini wakati huu zikisalia mechi 11 pekee

Kocha wa Chelsea, Antonio Conte akishangilia baada ya timu yake kuibuka na ushindi dhidi ya West Ham. Machi 6, 2017
Kocha wa Chelsea, Antonio Conte akishangilia baada ya timu yake kuibuka na ushindi dhidi ya West Ham. Machi 6, 2017 Reuters / Toby Melville Livepic

Kocha wa klabu ya Chelsea ya nchini Uingereza, Muitaliano Antonio Conte, amewaambia wachezaji wake kuwa makini zaidi kwenye mechi zijazo baada ya ushindi dhidi ya West Ham wa mabo 2-1, ushindi uliowafanya kuongoza ligi kuu ya Uingereza kwa alama 10.

Matangazo ya kibiashara

Chelsea kama inavyofahamika kwa jina la utani The Blues, inaongoza mbele ya klabu ya Tottenham kwa alama 10 huku zikiwa zimesalia mechi 11 pekee ligi imalizike.

Mashabiki wa timu hiyo walikuwa wakiimba "tutashinda kombe la ligi" lakini kocha wao Conte anasema wanahitaji kupata alama nyingine 26 na hivyo kuanzia sasa watakuwa wanaenda hatua kwa hatua.

Alama hizi 26 zinamaanisha klabu hii itafikisha alama 92 huku ikiwa Tottenham itashinda mechi zake zote, itafikisha alama 89 pekee.

Licha ya kushuhudia timu yake ikipata ushindi wa 21 msimu huu, kocha Conte amesema hakufurahisha kwa sababu timu yake iliruhusu bao kwenye mchezo huo.

Winga Eden Hazard ndie alikuwa mwiba kwa West Ham, ambapo alitumia vema pasi ya Diego Costa kuiandikia timu yake bao katika dakika ya 25 kabla ya Diego Costa mwenyewe kuifungia timu yake bao la pili dakika za mwanzo kipindi cha kwanza.

Katika hatua nyingine kocha wa West Ham, Slaven Bilic amesema hatarajii kuona mahasimu wao klabu ya Chelsea ikipoteza mechi zilizosalia.