MUZIKI-GEORGE MICHAEL

Uchunguzi wa mwili wa mwanamiziki George Michael wakamilika, sasa anaweza kuzikwa

Picha ya George Michael, ikionekana kwenye sehemu ambayo mashabiki wake wameweka maua kwa kumbukumbu yake. December 27, 2016.
Picha ya George Michael, ikionekana kwenye sehemu ambayo mashabiki wake wameweka maua kwa kumbukumbu yake. December 27, 2016. REUTERS/Neil Hall/File Photo

Mwanamuziki wa pop raia wa Uingereza, George Michael, ambaye alikutwa amekufa nyumbani kwake siku ya Christimas, alikufa kwa sababu za kawaida, imesema ripoti ya uchunguzi.

Matangazo ya kibiashara

Wataalamu wanasema kuwa kifo chake kimesababishwa na moyo kushindwa kusukuma damu ilivyo kawaida pamoja na ini lake kuwa lilivimba, amesema Darren Salter, mganga mkuu wa hospitali ya Oxfordshire.

Salter amesema kuwa uchunguzi wa kifo chake umekamilika na hakuna haja tena ya kufanya uchunguzi zaidi.

Uchunguzi wa awali kwa mwili wa Michael aliyekuwa na umri wa miaka 53, na aliyepata mafanikio ya miaka 35 ya muziki, ulionesha kuwemo kwa kiwango cha dawa za kulevya na kutaka uchunguzi zaidi ufanyike.

Ugonjwa wa Dilated cardiomyopathy, ambao unaweza kusababishwa na matumizi makubwa ya dawa za kulevya, unaathiri moyo kusukuma damu katika hali ya kawaida na mishipa inatanuka.

Mshirika wa Michael, Fadi Fawaz amesema alimkutan mwenzake akiwa amelala kwa amani kitandani kwake mjini Gorin magharibi mwa jiji la London.

Hii inamaanisha kuwa mazishi ya mwanamuziki huyu sasa yanaweza kufanyika baada ya miezi mitatu ya uchunguzi.

Akizaliwa na Georgios Kyriacos Panayiotou baba mwenye asili ya Ugiriki na mama raia wa Uingereza, alizalia jijini London mwaka 1963, baadae alijiunga na bendi ya Wham na kuuza album zaidi ya 100.