EUROPA LEAGUE 2017

Kocha Jose Mourinho akosoa uwanja wa Rostov, asema haufai kwa mechi

Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho.
Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho. Reuters/Robert Pratta

Kuelekea mchezo wake wa hatua ya 16 bora ya michuano ya kombe la Europa, kocha mkuu wa klabu ya Manchester United ya Uingereza, Jose Mourihno, ameukosoa uwanja wa klabu ya Rostov ya Urusi, akihoji ikiwa mchezo wao unaweza kuchezwa kwa hali ya uwanja ilivyo.

Matangazo ya kibiashara

Mourihno amesema kuwa haamini kama ataenda kucheza mchezo huo, matamshi aliyoyatoa wakati wa mkutano wake na waandishi wahabari.

Kocha Jose Mourihno amesema kuwa, anafahamu itabidi wachezo mchezo wao, lakini ni vigumu kuamini kuwa watacheza kwenye uwanja ambao anasema haustahili kuchezewa mechi kubwa.

Mourinho ameufananisha uwanja wa Rostov na ule wa Olimp-2 sawa na ule wa Beijing wa Bird Nest ambao klabu hiyo na wenzao wa Manchester City walikataa kuutumia kwenye mchezo wao wa kirafiki.

Mourinho amesema kuwa kwa sasa anafikiria sana nini cha kufanya na kwamba alitarajia kuona uwanja ambao unaweza kutumika kwa kuchezea.

Kwa aina ile ile ya uwanja kama ule wa Beijing, binafsi na Manchester City tuliamua kutocheza, lakini kwa hapa inavyoonekana ni kuwa tutalazimika kucheza.

Kocha huyo amesema kuwa alizungumza na maofisa wa UEFA kuhusu hali ya uwanja ilivyo lakini akapuuzwa.

Amesema amesikitishwa na majibu wa afisa mmoja wa UEFA aliyezungumza naye, ambaye alimwambia kuwa wachezaji wanazo bima na hivyo hakukuwa na sababu za kuahirisha mchezo wao.