Michael Essien kuchezea Indonesia
Klabu ya Persib Bandung ya Indonesia imetangaza kuwa imemnunua mchezaji wa kimataifa wa Ghana Michael Essien. Hata hivyo klabu hiyo haikupendelea kutangaza kiwango cha fedha alichonunuliwa Essien.
Imechapishwa:
Essien ambaye ni mchezaji wa zamani wa Chelsea, AC Milan na Real Madrid, atakua mchezaji wa kwanza wa soka kujiunga katika ligi ya Indonesia tangu mwaka 1990.
Katika miaka ya 1990, mchezaji wa Cameroon Roger Milla na Mario Kempes wa Argentina walijiunga na ligi ya nchi hii.
Essien, mwenye umri wa miaka 34, amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuichezea klabu ya Persib Bandung, moja ya klabu bora nchini Indonesia.
Essien alikuwa mpaka hana klabu anayochezea tangu kuondoka katika klabu ya Panathinaikos mwishoni mwa msimu uliopita.
Klabu ya Persib Bandung, ambao ilimaliza ikiwa kwenye nafasi ya tano katika michuano ya msimu uliopita, haikupendelea kutangaza kiwango cha fedha alichonunuliwa kiungo huyo wa kati.