MALI-FIFA

Fifa yaifungia nchi ya Mali kujihusisha na masuala ya soka kwa muda usiojulikana

Rais wa shirikisho la mpira wa miguu duniani, Fifa, Gianni Infantino.
Rais wa shirikisho la mpira wa miguu duniani, Fifa, Gianni Infantino. Reuters

Chama cha soka nchini Mali, FEMAFOOT, kimefungiwa rasmi na shirikisho la soka duniani Fifa hadi pale maelekezo mengine yatakapotolewa, baada ya Serikali kuingilia masuala ya soka.

Matangazo ya kibiashara

Uamuzi huu wa Fifa umechukuliwa baada ya waziri wa michezo wa Mali, Houssein Amion Guindo, kutangaza kuwafukuza ofisini kamati ya utendaji ya chama cha soka nchini humo, FEMAFOOT.

Baada ya uamuzi wake, waziri Guindo alitangaza pia kuunda kamati ya mpito ambayo itakuwa inasimamia shughuli za kiutendaji za chama hicho cha soka na kutangaza kuitisha uchaguzi baada ya miezi 12.

Fifa inasema kuwa adhabu hiyo ya kufungiwa itaondolewa wakati Serikali itakapowarejesha madarakanim viongozi wa shirikisho hilo ikiwemo bodi ya shirikisho hilo na rais wake Boubacar Baba Diarra.

Taarifa ya Fifa imesema kuwa “Hakuna timu yoyote kutoka Mali, vikiwemo vilabu, vinaweza kushiriki kwenye mashindano ya kimataifa kuanzia Machi 17 hadi pale adhabu hii itakapoondolewa.

“Hii ina maana kuwa sio FEMAFOOT au mwanachama yoyote au afisa yoyote kutoka Mali atakayenufaika na miradi ya maendeleo, kozi au mafunzo kutoka Fifa au kutoka shirikisho la soka barani Afrika.