EUROPA LEAGUE

Man United yapangiwa kucheza na Anderlecht robo fainali ya Europa League

Kiungo wa Manchester united, Paul Pogba, akivua jezi yake kuigawa kwa mashabiki wa timu hiyo.
Kiungo wa Manchester united, Paul Pogba, akivua jezi yake kuigawa kwa mashabiki wa timu hiyo. Reuters/Phil Noble Livepic

Baada ya kumalizika kwa hatua ya 16 bora ya michuano ya Europa League barani Ulaya juma hili, hatimaye droo ya hatua ya robo fainali imetolewa na shirikisho la soka barani Ulaya UEFA.

Matangazo ya kibiashara

Klabu ya Manchester United ambayo usiku wa Alhamisi wa Machi 16 ilichomoza na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Rostov ya Urusi, imepangiwa kucheza hatua ya robo fainali na mabingwa wa ligi ya Ubelgiji klabu ya Anderlecht.

United ambayo watu wengi wanaipa nafasi sana kwenye michuano ya mwaka huu, ndio klabu pekee kutoka nchini Uingereza iliyobakia kwenye michuano hii baada ya wenzao Tottenham kutolewa.

Kikosi cha kocha Jose Mourinho kinatarajia kufanya vizuri kwenye hatua hii ingawa kocha huyu bado hakipi nafasi kikosi chake kufanya vizuri.

Klabu ya Ufaransa ya Lyon yenyewe itacheza na Besiktas, huku miamba ya Uholanzi klabu ya Ajax yenyewe itakutana na wajerumani klabu ya Schalke, wakati Celta Vigo watawakabili Genk ya Ubelgiji.

Mzunguko wa kwanza wa michuano hii unatarajiwa kupigwa Alhamisi ya Aprili 13 na marudiano kupigwa wiki inayofuata.

Ratiba Kamili:

Anderlecht (Ubelgiji) vs Manchester United (Uingereza)

Celta Vigo (Uhispania) vs Genk (Ubelgiji)

Ajax (Uholanzi) vs Schalke (Ujerumani)

Lyon (Ufaransa) vs Besiktas (Uturuki)