SOKA

Algeria yapata rais mpya wa Shirikisho la soka

Rais mpya wa Shirikisho la soka nchini Algeria Kheireddine Zetchi
Rais mpya wa Shirikisho la soka nchini Algeria Kheireddine Zetchi Wikipedia

Rais mpya wa Shirikisho la soka nchini Algeria Kheireddine Zetchi amesema kazi yake ya kwanza baada ya kuchaguliwa katika wadhifa huo ni kurejesha ubora wa timu ya taifa ya soka.

Matangazo ya kibiashara

Zetchi alichaguliwa bila kupingwa siku ya Jumatatu baada ya Mohamed Raouraoua, kukataa kuwania kwa muhula wa tatu.

Rais huyo mpya, amesema ana nia ya kumpata kocha mpya wa timu ya taifa kwa muda wa wiki mbili baada ya kujiuzulu kwa George Leekens raia Ubelgiji baada ya kuondolewa katika michuano ya mataifa bingwa barani Afrika mwezi Januari nchini Gabon.

Mbali na kuimarisha timu ya taifa, rais huyo mpya amesema  lengo lake lingine ni kuimarisha soka la nyumbani.

Raouraoua, amemaliza muda wake baada ya kuongoza soka nchini humo kwa miaka 12, muda ambao  wachambuzi wa soka wanasema alijitahidi sana kuimarisha soka la Algeria kimataifa.