CAF-SOKA

CAF yatangaza droo ya hatua ya mwondoano taji la Shirikisho

Nembo ya taji la klabu bingwa barani Afrika
Nembo ya taji la klabu bingwa barani Afrika Courtesy of CAF

Shirikisho la soka barani Afrika CAF, limetangaza droo ya hatua ya mwondoano, kufuzu hatua ya makundi kuwania taji la Shirikisho barani Afrika.

Matangazo ya kibiashara

Vlabu 16 vitakavyofuzu baada ya mechi za nyumbani na ugenini vitafuzu katika hatua ya makundi.

Kutakuwa na makundi manne, kila kundi na vlabu vinne.

Mechi za kwanza zitachezwa kati ya tarehe 7-9 mwezi Aprili huku mzunguko wa pili zikichezwa kati ya tarehe 14-16.

Droo kamili:-
1.Young Africans Vs MC Alger
2.TP Mazembe Vs JS Kabylie
3.AC Léopards Vs Mbabane Swallows
4. FUS Rabat Vs MAS Fez
5. Enugu Rangers Vs ZESCO United
6. CF Mounana Vs Ivory Coast ASEC Mimosas
7. Rail Club du Vs Tunisia CS Sfaxien
8. Bidvest Wits Vs Smouha
9. CNaPS Sport Vs Recreativo do Libolo
10. KCCA Vs Al-Masry
11. Gambia Ports Authority Vs Al-Hilal Al-Ubayyid
12. AS Port-Louis 2000 Vs Tunisia Club Africain
13. Rivers United Vs Rwanda Rayon Sports
14. Barrack Young Controllers Vs SuperSport United
15. AS Tanda Vs Platinum Stars
16. Horoya Vs Morocco IR Tanger