SOKA-AFCON 2019

Djibouti yapata ushindi wake wa kwanza tangu mwaka 2007

Nembo ya Shirikisho la soka barani Afrika CAF
Nembo ya Shirikisho la soka barani Afrika CAF cafoline

Djibouti imepata ushindi wa kwanza katika mchezo wa kimataifa wa soka tangu mwaka 2007.

Matangazo ya kibiashara

Ushindi huu ulikuja baada ya kuifunga Sudan Kusini mabao 2-0 Jumatano usiku katika mchuano wa awali, kufuzu katika hatua ya makundi, kutafuta tiketi ya kucheza fainali ya mataifa bingwa barani Afrika mwaka 2019 nchini Cameroon.

Mabao ya Djibouti yalitiwa kimyani na Hamza Abdi Idelh na Med Salam.

Katika mechi nyingine, Madagascar iliishinda Sao Tome e Principe bao 1-0 jijini Antananarivo.

Michuano hii inachezwa nyumbani na ugenini.

Siku ya Ijumaa, Comoros nao watakuwa nyumbani mjini Moroni kumenyana na Mauritius, huku mchuano wa marudiano ukipangwa kufanyika mapema wiki ijayo.

Mshindi kati ya Sao Tome and Principe na Madagascar, atafuzu katika kundi la A ambalo lina Senegal, Equatorial Guinea na Sudan.

Naye mshindi kati ya Sudan Kusini na Madgascar atafuzu kucheza katika kundi la B, pamoja na Cameroon, Morocco na Malawi.

Nalo kundi la C ambalo tayari lina Mali, Gabon, Burundi na Burundi linamsubiri mshindi kati ya Comoros na Mauritius.

Hata hivyo, katika mechi zote za kufuzu miaka iliyopita, imekuwa ikifanya vibaya na kufungwa mabao 15. Imefanikiwa tu kufunga bao 1.

Mechi za hatua ya makundi zitaanza kutifua vumbi mwezi Juni mwaka huu na kumalizika mwaka 2018 mwezi Novemba.

Mshindi wa kwanza atafuzu katika fainali hizo pamoja na timu zingine tatu zitakazokuwa zimemaliza katika nafasi ya pili lakini kwa alama nzuri.

Kuna makundi 12, na kila kundi lina timu nne.