Jukwaa la Michezo

Afrika Mashariki yanawiri katika mashindano ya riadha ya nyika ya dunia

Sauti 23:37
Wanariadha wa Kenya baada ya kushinda taji la mbio za kupokezana kitambaa katika mashindano ya riadha nyika ya dunia yaliyofanyika Jumapili Machi 26 2017 jijini Kampala
Wanariadha wa Kenya baada ya kushinda taji la mbio za kupokezana kitambaa katika mashindano ya riadha nyika ya dunia yaliyofanyika Jumapili Machi 26 2017 jijini Kampala www.iaaf.org

Wanariadha wa Kenya wametamba katika makala ya 42 ya mashindano ya riadha ya Nyika ya dunia yaliyomalizika Jumapili jioni katika uwanja wa Uhuru wa Kololo jijini Kampala nchini Uganda. 

Matangazo ya kibiashara

Geoffrey Kamworor alitetea taji aliloshinda mwaka 2015 nchini China baada ya kumaliza mbio za Kilomita 10 kwa upande wa wanaume kwa muda wa dakika 28 na sekunde 24.

Nafasi ya pili ilimwendea Leonard Kiplimo Barsoton pia kutoka Kenya, huku Abadi Hadis kutoka Ethiopia akimaliza wa tatu na kushinda medali ya shaba.

Tunachambua mashindano haya kwa kina.