MAGONGO

Timu ya taifa ya wanawake ya mchezo wa magongo nchini Marekani yasema inabaguliwa

Maseneta 14 nchini Marekani wameiandika barua Shirikisho la mchezo wa kuteleza wa  magongo nchini humo kushughulikia kwa haraka malalamishi yanayoikumba timu ya taifa ya wanawake.

Timu ya taifa ya Marekani mchezo wa magongo  wa kuteleza
Timu ya taifa ya Marekani mchezo wa magongo wa kuteleza static01.nyt.com
Matangazo ya kibiashara

Timu ya taifa ya wanawake inadai kuwa inaonewa kuhusu  malipo ya marupurupu yao.

Wachezaji hao wanadai kubaguliwa na kulipwa mshahara mdogo ikilinganishwa na wenzao wa kiume.

Wanasisitiza kuwa ikiwa malalamishi yao hayatatekelezwa, watasusia mashindano ya dunia yanayoanza siku ya Ijumaa nchini humo.

Maseneta wamesema wameshtushwa na taarifa kuwa Shirikisho la mchezo huo linatumia Dola Milioni 3.5 kuimarisha mchezo huo lakini wachezaji wa kike wanabaguliwa.

Ripoti zimekuwa zikisema kuwa timu ya wanaume nao imetishia kususia mashindano ya dunia yatakayofanyika nchini Ufaransa mwezi Mei ikiwa matakwa ya wenzao hayatatekelezwa.