SOKA

Uganda Cranes yapata muundo mpya wa jezi yake

Rais wa Shirikisho la soka nchini Uganda (Katikati) na wadau wengine wakionesha mfano wa miundo ya jezi ya timu ya taifa ya soka
Rais wa Shirikisho la soka nchini Uganda (Katikati) na wadau wengine wakionesha mfano wa miundo ya jezi ya timu ya taifa ya soka www.fufa.co.ug

Shirikisho la soka nchini Uganda FUFA, limezindua rasmi kampeni ya kutangaza muundo mpya wa jezi za timu ya taifa ya Uganda Cranes.

Matangazo ya kibiashara

Rais wa Shirikisho la soka nchini humo Mhandisi Moses Magogo amesema timu ya taifa sasa itakuwa na jezi tisa (9) zenye miundo mbalimbali.

Jezi hizo mpya zitatumika wakati wa michuano mbalimbali za Kimataifa ndani na nje ya nchi hiyo.

Uganda kwa sasa inajiandaa katika michuano ya kufuzu katika fainali za CHAN mwaka 2018 nchini Kenya, AFCON nchini Cameroon na kombe la dunia nchini Urusi mwaka 2018.

Kampeni hiyo ya kuwafahamisha wapenzi wa soka nchini humo jezi, hizo ambazo rangi zinazotawala ni njano na nyekundu, inatarajiwa kumalizika tarehe 22 mwezi Aprili.

Mbali na timu ya taifa ya wanaume, timu ya tuafa ya wanwake na zile za chipukizi chini ya miaka 23, 20 na 17 nazo pia zitapata fursa ya kutumia jezi hizo.