SOKA

Vurugu zasitisha mchuano wa kirafiki kati ya Senegal na Ivory Coast

Mchuano wa Kimataifa wa kirafiki kati ya timu ya taifa ya soka ya Ivory Coast na Senegal ulisitishwa Jumatatu usiku katika uwanja wa Sebastiien-Charltey jijini Paris nchini Ufaransa.

Shabiki alivyomkabili mchezaji wa Senegal
Shabiki alivyomkabili mchezaji wa Senegal GOAL/Library
Matangazo ya kibiashara

Mzozo ullizuka katika dakika ya 88 ya mchuano huo baada ya mashabiki kuingia uwanjani.

Hadi kusitishwa kwa mchuano huo, Sadio Mane alikuwa ameifungia  Senegal bao la kwanza lakini Cyriac Gohi Bi akaisawazishia Ivory Coast dakika mbili baadaye.

Mashabiki waliingia uwanjani na kumlazimu refarii alyekuwa anachezesha mchuano huo Mfaransa Tony Chapron kuusitisha kwa sababu walinzi walionekana kulemewa na mashabiki waliofurika uwanjani.

Mbali na mchuano huo, mataifa mengine yamekuwa katika harakati za kujiimarisha kuelekea michuano ya kufuzu kombe la dunia mwaka 2018 na mashindano ya CHAN pamoja na fainali ya mataifa bingwa barani Afrika mwaka 2019 nchini Cameroon.

Matokeo ya Jumatatu Machi 27 2017

  • Jamhuri ya Afrika ya Kati 1-2 Gambia
  • Mauritania 2-1 Congo

Mechi za kirafiki Jumanne Machi 28 2017

  • Tanzania vs Burundi
  • Misri vs Togo
  • Afrika Kusini vs Angola
  • Cameroon vs Guinea
  • Msumbiji vs Lesotho
  • Morocco vs Tunisia