Arsene Wenger aseme hawezi kuwa kocha wa Arsenal milele
Imechapishwa:
Kocha wa klabu ya soka ya Arsenal nchini Uingereza Arsene Wenger, amesema hawezi kuwa kocha wa klabu hiyo milele.
Wenger ambaye amekuwa katika klabu hiyo mwaka 1996, amekuwa akipata shinikizo za kujiuzulu kutokana na matokeo mabaya katika klabu hiyo.
Mashabiki wa Arsenal nao wamekuwa wakilalamika kuwa, wamesubiri taji la ligi kuu nchini kwa miaka 13 bila mafanikio.
Wenger amesema hata akiendelea kuwa katika klabu hiyo kwa wiki mbili au miaka miwili, hatabadilisha mfumo anaotumia kufunza soka.
Mbali na hatima yake katika klabu hiyo, Wenger amesema kuwa ana imani kuwa wachezaji wake Alexis Sanchez na Mesut Ozil wataendelea kuichezea klabu hiyo.
Kocha huyo ametoa kauli hiyo baada ya kuwepo kwa madai kuwa wachezaji hao wawili ambao mikataba yao itamalizika mwezi Juni mwaka 2018, wataondoka katika klabu hiyo.