MADAGASCAR

Madagascar yampata rais mpya wa Shirikisho la soka

Rais mpya wa Shirikisho la soka nchini Madagascar Doda Andriamiasasoa (Kushoto)
Rais mpya wa Shirikisho la soka nchini Madagascar Doda Andriamiasasoa (Kushoto) Wikipedia

Doda Andriamiasasoa ndio rais mpya wa Shrikisho la soka nchini Madagascar kuelekea Uchaguzi mpya utakaofanyika mwaka 2018.

Matangazo ya kibiashara

Doda amechukua nafasi ya Ahmad Ahmad ambaye mwezi huu alifanikiwa kuchaguliwa kuwa rais wa Shirikisho la soka barani Afrika CAF.

Hadi kuteuliwa kwake, Doda alikuwa Makamu wa rais wa Shirikisho hilo na amepewa jukumu la kusimamia soka nchini humo kwa muda.

Amekuwa katika uongozi wa soka nchini humo tangu mwaka 2003.

Aidha, amewahi kuwa mchezaji wa klabu ya Club des Finances na kuunda klabu yake inayofahamika kuwa DSA.

Barani Afrika, ameendelea kuwa Kamisa wa Shirikisho la soka barani Afrika CAF.