SOKA

Mchezaji wa Kenya aishtaki klabu ya Afrika Kusini Golden Arrows, FIFA

Clifton Miheso, mchezaji wa Kenya
Clifton Miheso, mchezaji wa Kenya Wikipedia

Mchezaji wa Kimataifa wa timu ya taifa ya soka ya Kenya Harambee Stars Clifton Miheso, amefungua mashtaka katika Shirikisho la soka duniani FIFA dhidi ya klabu ya Golden Arrows ya Afrika Kusini.

Matangazo ya kibiashara

Miheso amekuwa akidai kuwa uongozi wa klabu hiyo, ulimtishia kwa bastola kusitisha mkataba wake na klabu hiyo.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24, ameitaka FIFA kuichukulia hatua klabu hiyo na kumlipa Dola za Marekani 22,000 ambazo anasema anaidai klabu hiyo.

Miheso amekuwa akiichezea Harambee Stars na hadi sasa amecheza mechi 14 na kufanya mabao matano.