SOKA-UEFA

Ancelotti asema Bayern Munich inaweza kupindua matokeo dhidi ya Real Madrid

Cristiano Ronaldo alivyofunga dhidi ya Bayern Munich katika mchuano wa robo fainai klabu bingwa barani Afrika Aprili 13 2017
Cristiano Ronaldo alivyofunga dhidi ya Bayern Munich katika mchuano wa robo fainai klabu bingwa barani Afrika Aprili 13 2017 Reuters / Michaela Rehle Livepic

Kocha wa klabu ya Bayern Munich nchini Ujerumani, Carlo Ancelotti amesema ana imani na matumaini kuwa wachezaji wake wana uwezo wa kubadilisha matokeo baada ya kufungwa na Real Madrid ya Uhispania mabao 2-1 katika mzunguko wa kwanza wa hatua ya robo fainali kuwania taji la klabu bingwa barani Ulaya UEFA.

Matangazo ya kibiashara

Mchuano huo uliochezwa katika uwanja wa Bernabeu mjini Madrid, ulikuwa muhimu sana kwa mshambuliaji Ronaldo aliyefunga mabao mawili na kufikisha idadi ya mabao aliyoifungia klabu yake kuwa  100.

Mechi ya marudiano ni siku ya Jumanne wiki ijayo katika uwanja wa Allianz Arena, mjini Munich.

Bayern wanahitaji kupata ushindi wa mabao 2-0 ili kujihakikishia nafasi ya kusonga mbele katika hatua ya nusu fainali.

Ancelotti amesema, vijana wake hawana nafasi kubwa lakini bado wanaweza kufanya maajabu katika mchuano huo  watakaocheza nyumbani.

Matokeo mengine ya wiki hii michuano ya robi fainali.

  • Atletico Madrid (Uhispania) 1 vs 0 Leicester City (Uingereza)
  • Borrusia Dortmund (Ujerumani) 2 vs 3 Monaco ( Ufaransa)
  • Juventus (Italia) 3 vs 0 Barceona (Uhispania)