SOKA-ALGERIA

Lucas Alcaraz ateuliwa kuwa kocha mpya wa Algeria

Lucas Alcaraz, kocha mpya wa timu ya soka ya Algeria
Lucas Alcaraz, kocha mpya wa timu ya soka ya Algeria AFP PHOTO / JOSE JORDAN

Lucas Alcaraz ameteuliwa kuwa kocha mpya wa timu ya taifa ya soka ya soka ya Algeria.

Matangazo ya kibiashara

Shirikisho la soka nchini humo limetoa tangazo hilo siku ya Alhamisi na kusema kuwa raia huyo wa Uhispania mwenye umri wa miaka 50, anachukua nafasi ya Georges Leekens, aliyeondoka katika klabu hiyo mwezi Februari mwaka huu, baada ya matokeo mabaya katika michuano ya mataifa bingwa barani Afrika nchini Gabon.

Kabla ya uteuzi huo alikuwa anaifunza klabu ya Granada katika ligi kuu ya La Liga nchini Uhispania.

Kazi kubwa ya kocha huyu ni kuiongoza Algeria kufuzu katika fainali ya kombe la dunia mwaka 2018 nchini Urusi.

Algeria ambayo ipo katika kundi moja na Nigeria, Cameroon na Zambia, ni ya mwisho katika kundi hilo baada ya kutopata ushindi katika mechi mbili ilizocheza.

Mechi nne bado hazijachezwa.