SOKA-SUDANI-KUSINI

Uchaguzi wa Shirikisho la soka Sudan Kusini waahirishwa

Mali ikisheherekea bao la Abdoulay Diaby nchini Sudan Kusini.
Mali ikisheherekea bao la Abdoulay Diaby nchini Sudan Kusini. ALBERT GONZALEZ FARRAN / AFP

Uchaguzi wa Shirikisho la soka nchini Sudan Kusini uliokuwa umepangwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu, umeahirishwa kwa sababu za kisiasa.

Matangazo ya kibiashara

Rais wa zamani Chabur Goc Alei, amedai kuwa Kamati itakayosimamia Uchaguzi huu imeonekana ikipata ushawishi kutoka kwa wabunge wa chama tawala wa SPLM, na Magavana wa chama hicho, wanaotaka mgombea wao achaguliwe.

Mbali na Chabur, kuna ripoti ya baadhi ya wanachama wa Kamati kuu ambao wamelinadikia barua Shirikisho la soka duniani FIFA, kulalamikia suala hili.

Wadau wa soka nchini Sudan Kusini sasa wanaiomba FIFA kuisaidia kuandaa Uchaguzi huu utakaokuwa huru na haki.

Uchaguzi huu unatarajiwa kufanyika baada ya aliyekuwa rais, kuondolewa katika wadhifa huo kwa madai ya ufisadi na baadaye akaamua kujiuzulu.

Shirikisho la soka nchini humo SSFA, kilizinduliwa mwaka 2012 na baadaye kujiunga na FIFA, CAF na CECAFA.