SOKA-ARSENAL-MAN CITY

Arsenal yailaza Manchester City kwa 2-1

Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger akisalimia na mchezaji wake Alexis Sanchez anayeripotiwa kutofautiana na kocha wake, na ambaye aliipeleka timu yake fainali kwa goli alilofunga katika dakika ya 101
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger akisalimia na mchezaji wake Alexis Sanchez anayeripotiwa kutofautiana na kocha wake, na ambaye aliipeleka timu yake fainali kwa goli alilofunga katika dakika ya 101 Reuters / John Sibley Livepic

Klabu ya Arsenal imetinga fainali ya kombe la kombe FA baada ya kuwaburuza Manchester City kwa mabao 2-1 katika mchuano wa nusu fainali uliopigwa siku ya Jumapili Aprili 23.

Matangazo ya kibiashara

Ushindi huo umepelekea Arsenal kuifuata ta Chelsea katika fainali ya FA. Mchezo huo wa nusu fainali ulichukua dakika 120 baada ya timu hizo kutoshana nguvu kwa sare ya bao 1-1 katika dakika tisini za muda wa kawaida.

Alexis Sanchez aliipeleka timu yake fainali kwa goli alilofunga katika dakika ya 101, kwa kufuatia patashika ya mpira wa kutengwa iliyotokea kwenye goli la City, baada ya timu hizo kuwa sare ya bao 1-1.

Man City ndio walioanza kuliona lango la Arsenal kwa goli la dakika ya 62 liliowekwa wavuni na mshambuliaji wake Sergio Aguero Kun.
Beki wa Arsenal Nacho Monreal alisawazisha bao hilo katika dakika ya 71.

Fainali ya mchezo wa kombe la FA itapigwa Mei 27 katika uwanja wa Wembley kati ya Arsenal na Chelsea.