SOKA-REAL MADRID-ATLETICO MADRID

Nusu fainali ya kwanza ya michuano ya klabu bingwa Ulaya kupigwa Jumanne hii

Real Madrid kumenyana na Atletico Madrid leo Jumanne Mei 2 katika uwanja wa Estadio Santiago Bernabeu.
Real Madrid kumenyana na Atletico Madrid leo Jumanne Mei 2 katika uwanja wa Estadio Santiago Bernabeu. REUTERS/Andrea Comas

Michuano ya klabu bingwa Ulaya hatua ya nusu fainali inaanza Jumanne hii kwa mchezo mmoja ambapo Real Madrid itaivaa Atletico Madrid klabu bingwa Ulaya. Wakati huo huomMechi fainali ya pili inawakutanisha FC Monaco dhidi ya Juventus, wakati ambapo mechi za kwanza zikitarajiwa kupigwa Mei 9 na 10.

Matangazo ya kibiashara

Hii ni mara ya 5 kwa Timu hizi kupambana katika Mechi za Ulaya.

Real Madrid wana matumaini ya kufanya vizuri na kuzima ndoto za Atlético Madrid kwenye michuano hiyo.

Real Madrid walifanya vizuri katika Misimu Mitatu iliyopita, ikiwa ni pamoja wa Fainali za Mwaka 2014 na 2016.

Mchezo huo utapigwa Jumanne hii usiku katika uwanja wa Estadio Santiago Bernabeu Jijini la Madrid, nchini Uhispania.

Hayo yakijiri Manchester United ambayo inatarajiwa kucheza mchezo wake wa kwanza wa nusu fainali ya ligi kuu ya Ulaya siku ya Alhamisi, inaweza kuwakosa nyota wake saba wa kikosi cha kwanza.

Wachezaji hao ambao wanaweza kukosekana katika mchezo huo ni pamoja na Bailly au Chris Smalling pamoja na Phil Jones ,wengine ni Zlatan Ibrahimovic, marcos Rojo na Tomothy Fosu-Mensah.

Hata hivyo Paul Pogba anatarajiwa kurejea katika mchezo huo utakaofanyika nchini Uhispania baada ya kukosa mechi mbili kutokana na kuwa na majeruhi.