TANZANIA-SOKA

Serengeti Boys ya Tanzania kumaliza kazi na Cameroon kabla ya kwenda Gabon

Kikosi cha Serengeti Boys nchini Tanzania
Kikosi cha Serengeti Boys nchini Tanzania Twitter TFF

Timu ya taifa ya soka ya Tanzania ya wachezaji chini ya miaka 17, inayofahamika kama Serengeti Boys usiku wa Jumatano unacheza mechi ya marudiano ya kirafiki na Cameroon. 

Matangazo ya kibiashara

Mechi hiyo itachezwa jijini Yaounde. Mchuano wa kwanza, Tanzania iliponyoka na ushindi wa bao 1-0.

Baada ya mchuano huu,vijana wa Serengeti Boys watasafiri kwenda jijini Libreville nchini Gabon kujiweka tayari kwa michuano ya kuwania ubingwa wa Afrika.

Kabla ya kupiga kambi nchini Cameroon, Serengeti Boys walikuwa katika maandalizi mengine nyingine mjini Rabat nchini Morocco.

Matokeo ya mechi za kirafiki kuelekea fainali hii:-

  • Tanzania 2-1 Gabon
  • Tanzania 3-0 Burundi
  • Tanzania 2-0 Burundi
  • Tanzania 2-2 Ghana

Fainali hii itafungua milango yake tarehe 14, kati ya wenyeji Gabon watakaomenyana na Guinea mjini Franceville, huku Cameroon wakipambana na Ghana.

Tanzania itaingia uwanjani katika mchuano wake wa kwanza dhidi ya Mali tarehe 15, huku mataifa mengine katika kundi hili la B, Angola na Niger wakipambana baadaye siku hiyo.

Mataifa manane yanashiriki katika makala haya ya 17 huku mataifa manne yatakayofuzu katika hatua ya nusu fainali, yakifuzu kuliwakilisha bara la Afrika katika michuano ya dunia nchini India mwezi Oktoba mwaka huu.