UEFA-MONACO-JUVENTUS-SOKA

UEFA: Monaco yasalimu amri nyumbani kwa kufungwa na Juventus 2-0

Gonzalo Higuain a été très efficace face à Monaco en demi-finale aller de la Ligue des champions. L'Argentin a inscrit les deux buts de la Juventus.
Gonzalo Higuain a été très efficace face à Monaco en demi-finale aller de la Ligue des champions. L'Argentin a inscrit les deux buts de la Juventus. Eric Gaillard/Reuters

Klabu ya Juventus imetamba ugenini katika dimba la Louis II dhidi ya AS Monaco kwa kuifunga 2-0 katika nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa. Mabao yote mawili ya Juventus yamefungwa na Gonzalo Higuain.

Matangazo ya kibiashara

Klabu ya Monaco imesalimu amri kwa kukubali kufungwa nyumbani na Juventus kwa mabao 2-0.

Mabao ya ushindi ya Juventus yalifungwa na Mchezaji Gonzalo Higuain katika dakika ya 29 kipindi cha kwanza na bao la pili katika dakika ya 59 kipindi cha pili, na timu hizo zitarejeana tena mnamo mei 9 mwaka huu.

Baada ya michezo miwili ya nusu fainali ya kuchezwa utafuta mchezo wa fainali utakaopigwa June 3 mjini Cardiff ukizikutanisha timu zilizofuzu hatua ya nusu fainali.

Itafahamika kwamba katika hatu hiyo ya nusu fainali ya kwanza, timu kadhaa zimeshinda ikiwa ni pamoja na Real Madrid ambayo iliichapa Atletico Madrid.