CAF-SOKA-AHMED

Ahmed Ahmed: Nimekataa kuchukua mshahara kutoka CAF

Rais mpya wa shirikisho la Soka barani Afrika, Caf, Ahmed Ahmed.
Rais mpya wa shirikisho la Soka barani Afrika, Caf, Ahmed Ahmed. performgroup

Rais wa shirikisho la soka barani Afrika CAF, Ahmed Ahmed amesema kuwa amekataa kulipwa mshahara kutoka kwa shirikisho hilo hadi pale mambo yote yatakuwa yamewekwa wazi.

Matangazo ya kibiashara

Raia huyo wa Madagascar mwenye umri wa miaka 57 alisimamia mkutano wake mkuu katika shirikisho hilo siku ya Jumatatu kabla ya kufanyika kwa mkutano mkuu wa shirikisho la Fifa siku ya Alhamisi.

Maswala muhimu yatakayozungumziwa ni namna ya kuifanyia mabadiliko CAF.

''Nimekataa kuchukua mshahara kwa sababu sio heshima kwa usimamizi mzuri'', Bw Ahmed amewambia waandishi wa habari, huku akiongeza kuwa mishahara ya wafanyakazi wote wa Caf kutoka wasimamizi hadi maafisa wakuu na rais akiwemo inapaswa kuwa na uwazi''.

Bw Ahmed amesema mabadiliko kuhusu usimamizi ni swala muhimu sana. “Kila mtu anapaswa kujua kinachotendeka'', alisema Ahmed.

Uchaguzi waBw Ahmed katika uongozi wa CAF mnamo mwezi Machi ulimaliza uongozi wa miaka 29 wa aliyekuwa rais wa shirikisho hilo kutoka Cameroon Issa Hayatou.