FIFA

Rais wa FIFA asema wakosoaji wake hawataki mabadiliko yanayoendelea

Rais wa Shirikisho la soka duniani FIFA Giani Infatino
Rais wa Shirikisho la soka duniani FIFA Giani Infatino FIFA.COM

Rais wa Shirikisho la soka duniani FIFA Gianni Infantino amekosoa vikali watu wanaotoa taarifa za uongo kuhusu uongozi mpya na mbadiliko yanayofanywa.

Matangazo ya kibiashara

Akizungumza kwa hisia katika mkutano Mkuu wa FIFA wa 67 jijini Manama nchini Bahrain, Infatino amesema wale wanaosambaza taarifa za uongo ni wale wasiopenda mabadiliko yanaoendelea.

Infatino ambaye wakosoaji wake wanahoji uwezo wake wa kuleta mabadiliko ya kweli, amesema ufisadi hautashuhudiwa tena katika Shirikisho hilo.

Aidha, amesema kuwa uongozi wa sasa ni tofauti na uongozi uliopita ambao amesema unafanya kazi kwa uwazi.

Rais huyo pia amewataka viongozi wa soka kutoka maeneo mbalimbali duniani walio na nia ya kujitajirisha kupitia mchezo wa soka, waachane na mchezo wa soka.

Miaka ya hivi karibuni, FIFA ilikabiliwa na tuhma za ufisaidi na kusababisha aliyekuwa rais wa zamani Sepp Blatter kujiuzulu kwa madai ya matumizi mabaya ya fedha ya Shirikisho hilo.

Wakati uo huo, mkutano huo umeidhinisha kufungukiwa kwa Guatemala na Kuwait kwa sababu mbambali.

Guatemala imefungiwa kwa sababu za ufisadi huku Kuwait ikipewa adhabu kwa sababu serikali nchini humo iliingilia maswala ya usimamizi wa soka nchini humo.